Jumatatu, 4 Mei 2015

CHELSEA MABINGWA ENGLAND MARA YA 4


Vinara wa ligi kuu nchini England klabu ya Chelsea imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu nchini England msimu huu wa 2014/2015.

Chelsea wametawazwa mabingwa wapya baada ya kuwalaza Crystal Palace bao 1-0 pambano lililopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge darajani goli pekee la chelsea likifungwa na Eden Hazard kwa penati.

Kwa matokeo hayo Chelsea wametawazwa kuwa mabingwa wapya zikiwa zimebaki mechi 3 huku Chelsea ikifikisha pointi 83 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika msimamo.