Jumamosi, 25 Aprili 2015

YANGA HAO KIULAINI KOMBE LA LIGI KUU 2015


Ubingwa wa ligi kuu ya vodacom umesogea mpaka kwenye ubalaza wa yanga ukingoja pointi tatu katika michezo mitatu aliyobakisha kutwaa ubingwa huo, unaoshikiliwa na Azam FC.

Yanga SC  wametoa kichapo cha goli 5-0 kwa Ruvu shooting katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom, ambapo jana ulichezwa mchezo mmoja katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 Katika mchezo huo yanga walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-0, ambapo goli lao la kwanza lilipatikana katika dakika ya 9 ya mchezo kupitia kwa Saimon Msuva.

Mshambuliji toka Liberia Kpah Sherman aliendeleza utamaduni wa kuziona nyavu katika siku za karibuni, baada ya kuifungia yanga goli la pili hapo jana katika dakika ya 24.

Saimon Msuva alifunga goli lake la 16 msimu huu, likiwa ni goli lake la pili katika mchezo wa jana katika dakika ya 45, na kuipeleka yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3-0.

Katika kipindi cha pili yanga walipata magoli mawili kupitia kwa Kpah Sheman katika dakika ya 56 na Amisi Tabwe katika dakka ya 66 na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 5-0.

Kwa matokeo ya jana Yanga wameongeza wigo wa tofauti ya pointi baina yake na Azam FC toka katika 7 mpaka kufika 10, yanga wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Endapo leo Azam FC wakishindwa kupata matokeo kutapelekeaa Yanga kutawazwa mabingwa wa msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa wamebakiza michezo mitatu.

Azam Fc leo watakuwa wenyeji wa Stand united katika uwanja wa Azam complex, huku yanga wakitarajwa kushuka uwanjani jumatatu kuwakabili polisi morogoro.leo pia kuna michezo itaendelea  ambapo mbeya city toka mkoani mbeya watakuwa wanacheza na kagera sugar. na kule  manungu mtibwa sugar watakuwa wanawakaribisha jkt ruvu watoto minziro ,huku simba akicheza na ndanda fc