MKUU wa Wilaya ya Kisarawe SUBIRA MGALU amezindua Rasmi Shindanola Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitiaKampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika Kilimo nakumkwamua Kiuchumi.Akizungumza katika Sherehe hizo SUBIRA MGALU amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikiaWilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi Wakina Mamakuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa Wakina mama wa Kisarawesio Wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na Mshindi wakwanza atokee katika Wilaya hiyo.Ameongeza kuwa Shindano hilo linampa mwanamke uwezo wa kutambua haki
zake hasa za Umiliki wa Ardhi na kuongeza kuwa ni shindano ambalo
mshiriki anahitaji kuwa Mbunifu,Mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana
mawazo na kuwa na mbinu za kisasa za kilimo bora.