Alhamisi, 16 Aprili 2015

MAYWEATHER KUTUMIA DOLA ELFU ISHIRINI NA TANO ZA KIMAREKANI KULINDA MENO YAKE



Ikiwa zinahesabika siku na masaa kuelekea kwenye pambano linalosuriwa kwa hamu ulimwenguni kati mmarekani Floyd Mayweather na mfilipino Manny Pacquiao, Mayweather ameendelea kutamba na kumfanya azidi kuzungumziwa na vyombo vya habari duniani
Taarifa kutoka jarida la Forbes la nchini Marekani zinasema Mayweather atatumia kifaa cha kulinda meno (mouth Guard) chenye gharama ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano.