Jumamosi, 18 Aprili 2015

MANCHESTER UNITED KUWAKOSA WANNE LEO

Mastaa wanne wa Man United  kuwakosa Chelsea Leo
LOUIS VAN GAAL


Kipute cha ligi kuu nchini Uingereza kinaendelea leo hii ambapo macho na masikio ya mashabiki wengi yataelekezwa kwenye uwanja wa darajani Stamford ambapo timu ya Chelsea itawaalika mashetani wekundu timu ya Manchester United.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kikosi chake huenda kikawakosa nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza.
Van Gaal amewataja nyota hao ambao ni Michael Carrick, Marcos Rojo, Daley Blind na Phil Jones ambapo majereha bado yanawatesa.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia kwani pamoja na Chelsea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, Manchester United pia inanafasi ya kunyakua kikombe hicho endapo itamfunga Chelsea basi itapunguza uwiano wa point 8 walizopishana.
Michezo mingine itakayopigwa leo ni pamoja na Everton dhidi ya Burnley, Leicester City wakipambana na Swansea City, huku Stoke City wakimenyana na Southampton.