ZAKHEM FC /FFU SC, KUSAKA BINGWA WA JUMLA MICHUANO
YA LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM.
Baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi ya mkoa wa
Dar es salaam na kupata timu tatu zitakazouwakilisha mkoa katika michuano ya
ligi ya mabingwa ya mikoa ya TFF,kesho Alhamis Aprili 09/2015,katika uwanja wa
Karume jijini kutakuwa na mchezo wa fainali ya kumpata Bingwa wa jumla wa
michuano ya ligi ya mkoa.
Timu zitakazoumana katika fainali hiyo ni ZAKHEM FC
dhidi ya FFU SC,ambazo zitashuka dimbani majira ya saa kumi jioni zikishuhudiwa
na umati wa mashabiki waliokuwa wakiyafuatilia mashindano hayo tangu yalipoanza
kutimua vumbi.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka
mkoa wa Dar es salaam DRFA,timu zilizofanikiwa kuuwakilisha mkoa katika
michuano ya ligi ya maabingwa ni pamoja na ZAKHEM FC,FFU SC na CHANGANYIKENI
SC.
Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,ameipongeza kamati hiyo
ya mashindano kwa kusimamia vizuri uendeshaji wa ligi tangu ilipoanza.