Alhamisi, 23 Aprili 2015

JACOB ZUMA AAHIDI KUMALIZA CHUKI DHIDI YA WAGENI


RAIS JACOB ZUMA wa Afrika Kusini ameahidi kushughulikia tatizo la chuki dhidi ya wageni nchini humo, huku Wanajeshi wakipelekwa kusaidiana na polisi kuzima mashambulizi dhidi ya wageni yaliyouwa watu wasiopungua saba hadi sasa.
Wanaume 11 wamekamatwa katika operesheni ya pamoja kati ya Polisi na Jeshi kwenye bweni mjini Johannesburg, saa chache baada ya jeshi kuingilia kati.
Baada ya kukutana na Viongozi wa Kibishara, Kiraia na Kidini, ZUMA amesema Serikali yake itachukuwa hatua thabiti kushughulikia matatizo yanayosababisha mashambulizi, na kuhakikisha kuwa wageni hawalengwi tena