Jumapili, 14 Februari 2016

TZ PRISONS IMEILAZIMISHA MWADUI FC DROO TASA HUKO MWADUI HUKU AZAM FC AKICHAPWA NA COASTAL UNION

Timu ya Tz Prisons ya Mbeya leo hii Imeilazimisha timu ya Mwadui Fc nyumbani kwake sare ya bila kwa bila .na huko Tanga Azam Fc imeshindwa kuiengua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC, baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Shukrani zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, ambalo linavunja rekodi ya Azam Fc kutofungwa msimu huu, beki wa kulia Miraj Adam aliyetikisa nyavu.