Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo hii na kesho kwa michezo saba
kuchezwa katika viwanja tofauti, huku kila timu ikisaka pointi tatu
muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Leo, Uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga, Stand United
watawakaribisha Simba SC, Mgambo Shooting v African Sports (Mkwakwani),
Mbeya City v Toto Africans (Sokoine), Ndanda FC v Majimaji (Nangwanda)
na JKT Ruvu v Kagera Sugar uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mwadui Complex, huku Coastal Union wakicheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.