Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager imerejea jana jioni ikitokea chini Afrika
Kusini ilipokuwa imeweka kambi ya siku kumi, ambapo leo jioni itafanya
mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mzalendo Charles
Boniface Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la
Posta, na leo jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya
TP Mazembe ya Congo DR wameungana kambini na wachezaji wenzao jana na
kufanya kikosi cha Stars kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.
Wapinzani wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria wanatarajiwa
kuwasili leo saa 12 jioni nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na
kufikia katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni
Ijumaa watafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Wakati huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, mwamuzi wa
kati Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa
akiba Coulibaly Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi, huku
mtathimini wa waamuzi Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger
alishawasili nchini tangu juzi usiku.
Kamisaa wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini Zimbambwe
anawasili nchini leo mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini (South
Africa Airways