Jumatano, 11 Novemba 2015

MKUU WA WILAYA YA MBEYA AIGA STAILI YA MAGUFULI




IMEANDIKWA  NA:DAVID NYEMBE (FAHARI NEWS)

MKUU wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Sabi Mnasa, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya na kutaka wateja wote kuingizwa katika mfumo wa kompyuta.


 wafanyakazi wa mamlaka hiyo wamesema amewaongezea nguvu na hali ya kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu katika awamu hii ya Hapa Kazi Tu
KWA HISANI YA FAHARI NEWS