Ijumaa, 13 Novemba 2015

Mahakama ya nyumba yawahoji waliyo mnyang'anya nyumba ya mzee Isangu Arusha.


Hatimaye Mahakama ya ardhi na nyumba kanda ya Arusha imewaita kwa hati ya dharura Bi Janeth Fosbrooke na wakala wa mahakama Majembe Auction Mart wanaodaiwa kumwondoa kwa nguvu katika nyumba yake mzee Juma Isangu kwa ajili ya kujibu shitaka linalo wakabili.

Ilikuwa ni majira ya saa tano asubuhi katika mahakama ya ardhi na nyumba kanda ya Arusha ambapo mwenyekiti wa mahakama ya ardhi na nyumba  mkoa wa Arusha Cyriacus Kamugisha alisoma shitaka linalo wakabili Bi Janeth Fasbrooke na wakala wa mahakama Majembe Auction Mart lakini mwakilishi wa wakala wa mahakama alipo ulizwa alipata wapi ruhusa ya kuvamia na akatoa vyomba katika nyumba hiyo akatoa utetezi kuwa alifauta amri ya mteja wake na kwamba hausiki katika mgogoro huo.

Lakini mwenyekiti Kamugisha alilazimika kuahirisha shitaka ilo hadi jumatatu ya tarehe kumi na sita saa mbili asubuhi kutokana na Bi Janeth kushindwa kuhudhulia mahakamani kwa madai kuwa ni mgonjwa na mahakama kumtaka tarehe kumi na sita bila kukosa afike mahakani hapo.