Jumanne, 24 Novemba 2015

HATIMAYE TUMBA SWEDI LUO ATUA MBEYA CITY

tumba swedi--mccfc
Aliyekuwa mlinzi wa kutumainiwa wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Tumba Swedi Luo amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc.
Mapema leo kwenye ofisi la City zilizopo  jengo la Mkapa Hall jijini hapa Swedi ametia sini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu tayari kabisa  kuitumikia timu yake mpya kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na pia mashindano mengine.
Akizungumza mara baaada ya kutia saini kandarasi hiyo Swedi alisema kuwa amefurahi kujunga na timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa kwenye mpira wa Tanzania bara tangu aliponda ligi kuu huku akiahidi kufanya kazi kwa uwezo wake wote aliojaaliwa na Mungu kwa lengo la kuisaidia City kupata mafaniio zaidi kwenye ligi kuu.
“Nimefurahi kujiunga na City, hii ni timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa, tangu ilipopanda daraja imeleta changamoto nzuri na zaidi imekuwa timu ya ushindani na kutafuta mafanikio, hakika namshukuru mwenyezi mungu, hapa ni sehemu ambayo naweza kupata mafanikio zaidi, imani yangu kubwa ushirikino wa pamoja na niliowakuta hapa tutakuwa na mafanikio zaidi ya yale niliyokuta” alisema.
Tumba Swedi Luo kabla ya kujiunga na City alikuwa mchezaji wa Coastal Union kwa misimu miwili mfululizo  akicheza jumla michezo michezo  36 na kuisaidia  timu yake  hiyo ya zamani kushika nafasi tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya vodacom msimu uliopita.