Hili
Ndilo Soko Jipya la Mwanjelwa Soko la Kisasa ambalo ndilo linaleta
Mushikeli na wafanyabiashara, Ikumbukwe hapa ndipo ambapo paliungua.
Hapa
Maduka yote upande wa Sido yamefungwa, Pako Kimya kabisa huku
wafanyabiashara wote wakiwa katika mkutano na Halmashauri ya Jiji katika
Ukumbi wa Mkapa.
Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Samweli Lazaro akifafanua Jambo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Jiji
Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza akiwaeleza wafanyabiashara makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa
Mwenyekiti wa wafanya Biashara wa Mkoa wa Mbeya Charles Sionga akisisitiza jambo
Katibu wa wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya Allanus Ngogo akiuliza swali kwa niaba ya wafanyabiashara
Mmoja wa wafanyabiashara na Muhanga wa kuunguliwa na Soko la Mwanjelwa akiuliza swali
Wafanyabiashara wa Soko la Mwanjelwa wakiwa katika mkutano na Jiji
Picha na Mbeya yetu
WAHANGA wa Soko
la Mwanjelwa jijini Mbeya ambao wanafanyabiashara zao katika Soko la Sido
wameitaka Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutolifungua soko jipya hadi
watakapopata eneo mbadala.
Wafanyabiashara hao
wametoa kauli hiyo kufuatia Halmashauri kuwataka kujisajili kwa ajili ya
kuingia kwenye soko jipya baada ya ukarabati wake kukamilika.
Aidha
wafanyabiashara hao ambao ni wahanga wametakiwa kujaza fomu hizo hadi kufikia
Agosti 17 mwaka huu ili waanze kufanya biashara zao mara moja kutokana na
Halmashauri kuanza kulipa deni Agosti 30 mwaka huu.
Akizungumza
katika mkutano na Wahanga hao katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Mkapa,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Musa Zungiza alisema wamelazimika
kuanza kuwaruhusu mapema kutokana na kudaiwa mkopo uliotakiwa na Benki ya CRDB.
Zungiza alisema
Benki inaitaka Halmashauri kupitia soko hilo kulipa deni la Shilingi Bilioni 25
kwa muda wa miaka 15 deni linalotakiwa kuanza mapema mwaka huu ili kuendana na
kipindi hicho.
Alisema kutokana
na ukubwa wa deni hilo Halmashauri pamoja na uongozi wa Wafanyabiashara ambao
walipewa eneo la muda la Sido wamekubaliana kuwepo kwa utaratibu juu ya
upatikanaji wa fedha za kulipa deni hilo.
Alisema utaratibu
huo ni pamoja na kila mfanyabiashara atakayepewa chumba kwa ajili ya duka
atalazimika kulipia shilingi Laki tano kwa mwezi huku mwenye kizima akilazimika
kulipia ushuru wa shilingi 1000 kwa siku na wengine 15000 kutegemeana na
biashara.
Aliongeza kuwa
ili deni hilo liweze kupatikana na kukusanywa kwa wakati Halmashauri
imeikabidhi jukumu hilo shirika la UTT ambalo litakuwa na jukumu la kukusanya ushuru,
kusimamia usafi, umeme na huduma za maji ndani ya soko.
Alisema kwa
utaratibu huo Halmashauri itatakiwa kuilipa benki ya CRDB Shilingi
Milioni 341 kila mwezi kwa muda wa miaka 15 ili kukamilisha deni lote hivyo
kupitia wafanya biashara ambao ni wahanga ndiyo watakaolipa kupitia ushuru.
Akifafanua zaidi
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wafanyabiashara, Kwa niaba ya Mkurugenzi, Dk.
Samwel Lazaro alisema uaratibu wa soko hilo utawapa kipaumbele wahanga ambao
watatimiza masharti ya kulipa kiingilio ndipo watakapokaribishwa wengine.
Alisema wahanga
ambao watakosa fedha hizo watatafutiwa eneo mbadala ambalo watakubaliana nalo
kwa pamoja ili wahamie wote ikiwa ni pamoja na kuendelea katika eneo la sido
ambalo walitakiwa kuwepo kwa muda.
Kwa upande wao
wafanyabiashara hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Charles Syonga na Katibu
Alanus Ngogo waliowataka viongozi wa Halmashauri kutokulifungua soko jiopya
hadi pale eneo mbadala litakuwa limepatikana.
Walisema pia
wafanyabiashara wakipatiwa eneo waachiwe walijenge wenyewe pampoja na
kuandikishana mikataba ya kisheria ili kuepuka kuhamishwa hamishwa mara kwa
mara.
Akijibu maswali
hayo kwa niaba ya Mkurugenzi, Dk. Lazaro alisema eneo la Sido linamgogoro ambao
kesi yake iko mahakamani lakini wahanga hao hawataondoka eneo hilo hadi hapo
sehemu mbadala itakuwa imepatika.
Alisema kuhusu
eneo mbadala itategemea ni wahanga wangapi waliokosa sifa kwa Halmashauri
inawatambua waliounguliwa tu ambao ni 960 na sio zaidi ya hapo ambapo pia
alitoa wito kwa wafanyabiashara wengine kutumia mgongo wa wahanga kujipaia
maeneo.
Aliongeza kuwa
kuna baadhi yaw au wanatumia jina la Mkurugenzi kutapeli wafanyabiashara kwa
kuwalipisha fedha ili wapatiwe maduka jambo aliloswema ni utapeli na tayari
ameshakamatwa mmoja na kufikishwa polisi.