Jumatano, 12 Agosti 2015
YANGA YAENDELEZA DOZI KATIKA MICHEZO YA KUJIPIMA NGUVU MKOANI MBEYA
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wametoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons jioni ya leo katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe alianza kuifungia Yanga SC dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza , Malimi Busungu aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya tambwe aliipatia timu yake bao la pili na la ushindi dakika ya 84.
Mwinyi Haji wa Yanga SC na Zam Kuffoh wa Prisons, wote wawili walitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88 baada ya kupigana uwanjani.
kocha wa timu ya prisons alisema amegundua madhaifu ya timu yake katika mchezo wa leo dhidi yake na yanga pamoja na hayo amefurahishwa na mchezo wa leo umempa mbinu za kutengeneza kikosi cha kwanza kwa ajili ya kujiandaa na michezo mingine ya kujipima nguvu kabla ya kuanza ligi kuu tanzania bara.