Jumatatu, 17 Agosti 2015

MWIGAMBA AMCHUKULIA FOMU YA URAIS KITILA MKUMBO-ACT WAZALENDO

  Mwakilishi wa chama cha ACT WAZALENDO na Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akipewa maelekezo na Afisa tawala wandamizi wa Tume ya uchaguzi (NEC),George Baasha kuhusiana na vitu vinavyotakiwa kwenye uchaguzi mkuu pamoja na kampeni zitakazo anza hivi karibuni.
 Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akimwakilisha Dkt. Kitika Mkumbo  kupokea fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO amechukua fomu hizo leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.


 Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akionyesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO  mara baada ya kupokea fomu hiyo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu mkuu  wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.