Ijumaa, 24 Julai 2015

VITUKO VYATAWALA MCHAKATO WA KUWANIA UBUNGE NDANI YA CHAMA JIMBO LA MBEYA MJINI.


MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura
 SEHEMU ya wana-CCM wa kata ya Nsalaga 



MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga 
 akiomba kura





Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini, walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.




Vituko hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini kuomba kura.










Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano sasa.


























Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.









Makombe alisema akipewa ridhaa hiyo anao uhakika wa kulikomboa jimbo la Mbeya mjini, na baada ya kutekeleza hilo atahakikisha anatafuta wafadhiri watakaojenga viwanda ili viweze kutoa ajira kwa vijana mjini Mbeya.
KWA HISANI YA MBEYA YETU