Ijumaa, 24 Julai 2015

SAFARI YA KUJITAMBULISHA YA MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI KUTOKA CHATO MPAKA DODOMA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida. 
Wananchi wa Ikungi wakishangilia kwa ujio wa Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.