Jumatatu, 13 Julai 2015

Nec yatangaza majimbo 26 ya uchaguzi




Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva

Tume ya taifa ya Uchaguzi  (NEC),imetangaza kuanzishwa kwa majimbo mapya 26 kwa mujibu wa ibara ya 75(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya mwaka.

Akitangaza majimbo hayo mapya mapema leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa kwa mujibu wa ibara hiyo  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu la kuchunguza mgawanyo wa Jamhuri ya Muungano katika Majimbo yaUchaguzi;

Majimbo hayo ni kama ifuatavyo.

Majimbo 20 yanayoanzishwa kutokana na

kuanzishwa kwa

Halmashauri mpya ni:

1. Handeni Mjini 2. Nanyamba 3. Makambako 4. Butiama 5. Tarime Mjini 6. Tunduma 7. Nsimbo 8. Kavuu 9. Geita Mjini 10. Mafinga Mjini 11. Kahama Mjini 12. Ushetu 13. Nzega Mjini 14. Kondoa Mjini 15. Newala Mjini 16. Mbulu Mjini 17. Bunda Mjini 18. Ndanda 19. Madaba 20 Mbinga Mjini

MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA IDADI YA WATU NI KAMA IFUATAVYO.

Majimbo 6 yanayoanzishwa kutokana na idadi

ya watu ni:

1. Mbagala – Dar es salaam 2. kibamba – Dar es salaam 3. Vwawa – Mbeya 4. Manonga – Tabora 5. Mlimba – Morogoro6. Ulyankulu – Tabora