Mwenyekiti wa vijana mkoa wa mbeya Amani Kajuna leo ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la mbeya mjini kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Akiongea mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya hill view hotel amesema ni muda amepata fursa kuteta na watu mbalimbali ikiwa ni namna gani anaweza kuendesha maendeleo ya wana mbeya na kukuza uchumi wa jiji la mbeya na kwa mtu mmoja mmoja.
Aidha alisema endapo atachaguliwa na chama chake na baadae kupata nafasi ya kuliongoza jimbo la mbeya mjini ataondoa matatizo kodi zisizo na utaratibu mzuri,kupotea kwa michezo,kiwango cha elimu kushuka,watoto yatima Kukosa tumaini la maisha ya pamoja na watu wanaoishi katika mazingira magumu.