Mdau mkubwa wa michezo Mkoani Mbeya James Mwampondele amechukua Fomu ya kuomba kupata Ridhaa ya ubunge kupitia chama chake katika ofisi za ccm wilaya ya mbeya mjini moja ya Matukio makubwa ambayo ameyafanya mwampondele ni kujitolea kutengeneza magoli ya Netball katika viwanja mbalimbali vya shule za msingi vilivyopo jijini mbeya .ameweza kutoa msaada mkubwa wa kutengeneza uwanja wa sokoine kwa kupanda nyasi na gari lake kutoa nyasi toka Tukuyu na kuwezesha uwanja wa mpira kutumika katika michezo ya ligi kuu tanzania bara amekuwa ni mmoja wadau wakubwa wa kuchangia maendeleo ya vijana mmoja mmoja na vikundi mbalimbali ,ikiwemo kusaidia Kwaya mbalimbali za dini ,kusaidia sanaa kwa upande wa waigizaji ,mpira wa miguu kuzipatia jezi timu mbalimbali za jijini mbeya ikiwemo mipira ya miguu na netball.hata hivyo alisema endapo hata pata ridhaa ya kuchaguliwa na chama chake na baadae kupata nafasi ya kuchaguliwa na wananchi kuliongoza jimbo la mbeya mjini Atahakikisha anafuata Ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) na kuweza kuwasaidia wakazi wa jimbo la mbeya mjini kuwawezesha kupata Elimu ya kuendesha biashara ndogo ndogo na kuweza kuwafungulia Saccos za kuwakopesha vitu au pesa ili kuweza kuondokana na Tatizo la umaskini katika jimbo la mbeya mjini.