MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988 Coastal Union ya Tanga kesho Iddi Pili inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Friends Corner ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Iddi Pili kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa mechi za kujipima nguvu kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili ya mashindano ya Ligi kuu yajayo.
Maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na hivyo Friends Corner watatua mkoani siku hiyo hiyo ya mchezo huo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Taarifa inaeleza baada ya kumalizika mechi hiyo tutaangalie uwezekano wa kucheza mechi nyengine za majaribio ili kuweza kukipa makali kikosi cha timu hiyo ambacho msimu ujao kimedhamiria kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.
Na mtambue kuwa dhamira ya timu yetu ni kuhakikisha inafanya maandalizi kabambe ili kuweza kurejesha heshima yao ya miaka ya nyuma walipochukua ubingwa wa ligi kuu.
Hata hivyo tunawataka wanachama, wapenzi na mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo ili kuweza kuona viwango vya wachezaji wapya waliosajiliwa kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu.