Jumatatu, 11 Mei 2015

MKUTANO WA 20 WA BUNGE LA BAJETI KUANZA KESHO


MKUTANO wa 20 wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano,ambao ni maalamu kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali,unatarajiwa kuanza kesho mjini Dodoma.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa siku 39,utakuwa wa mwisho wa Bunge hilo kabla ya kuvunjwa na baadaye kufanyika uchaguzi Mkuu,Octoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge,Idara ya Habari kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,Mkutano huo utakuwa na maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa majibu,ambapo pia kutakuwa na wastani wa maswali 56,atakayoulizwa Waziri Mkuu na kuyapatia majibu.