
Uzinduzi wa mafunzo ya viongozi na wenyeviti serikali ya mtaa
ulifanyioka katika ukumbi wa PTA wiliya ya Temeke jijini Dar es Salaam,
uzinduzi wa mafunzo hayo ambayo yalifunguliwa rasmi na mwenyekiti Taifa
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA( Mh Freeman Mbowe
aliwataka viongozi hao na wenyeviti wa serikali za mitaa kuwa makini na
kufata kanunu za uongozi kwa kuwa na maadili safi kwani dhamana
waliyopewa na wanancho wao sio nafasi ya kufanya mchezo. Pia akitumia
mkutano huo kuwapongeza wale wote waliochaguliwa kuongoza serikali za
matiaa na kuwataka wafanye kazi kikamilifu katika ofisi zao kama
ilivyoonekana kupata mafanikio katika manispaa ya kinondoni kwa
kuongozwa na madiwani wa chadema jambo ambalo limeweza kuongeza kipato
cha manispaa hiyo. Akimtaka Naibu katibu Mkuu wa Bara Mh John Mnyika
kutaja takwimu la ongezeko hilo la ukusanyaji wa fedha jambo ambalo Mh
John Mnyika alimwita mwenyekiti wa Madiwani manispaa ya kinondoni Mh
Rosse Mushi na kueleza ongezeko la kipato hicho kutoka Billioni Saba
mpaka kufikia Billioni thelasini na tano, huku pato la ndani ukijumlisha
na mgao kutoka Serikali kuu ni shillingi Millioni saba na kwasasa
kufikia Billioni moja themanini na nne. Akisisitiza kutoridhishwa na
ongezeko hilo Mh John Mnyika aliwataka viongozi na wenyeviti wa serikali
za mitaa kuhakikisha wanaongeza nguvu kuhakikisha manispaa zinaongozwa
na chadema na meye pia na wabunge ili kuweza kuzibiti kipato cha
manispaa kikamilifu.
Mh Freeman Mbowe alieleza kuwa kipato cha Taifa kinategemea mkoa wa
Dar es Salaam ukiachilia mbali makao makuu ya serikali kuwa katika jiji
hili na ofisi nyingine nyeti kubwa, Akibainisha hayo pia alieleza idada
ya wapiga kura ambao ndio wanaipa dhamana chama gani kinachoweza
kuongoza Taifa na kuwaeleza kwa wingi za wapiga kura wa mkoa wa Dar es
Salaam ndio wenye dhaamana hiyo ya kuchagua chama gani kiongoze nchi.
akianza kutaja idadi ya wapiga kura alieleza jimbo la ubungo ndio
linalooongoza kuwa na wapiga kura wengi laki tano elfu sabini na tano
mia tatu sitini na sita, jimbo la pili ni jimbo la kigamboni lenye
wapiga kura laki nne elfu sabini na nane na thelasini, jimbo la tatu ni
jimbo Temeke lenye wapiga kura laki nne elfu kumi na saba mia nne na
thelasini na mbili, Jimbo la tatu ni segerea lenye wapiga kura laki nne
elfu kumi na moja mia sita na ishirini, Jimbo la nne ni jimbo la Kawe
lenye wapiga kura laki tatu elfu mia nne na themanini na tatu. jimbo la
tano ni Kinondoni lenye idadi ya wapiga kura laki tatu elfu mia sita na
sabini na nane. na jimbo la Ukonga lenye wapiga kura laki mbili elfu
selasini na tisa mia tatu na sabini na tano.
Akawaeleza nini maana ya takwim hizo ni kwamba idadi ya wapiga kura
wa mkoa wa Dar es Salaam ndio itadi kubwa kuliko mkoa wowote hivyo ni
muhimu kufanya kazi na kutengeneza mazingira mazuri ya ushindi
tunapoelekea uchaguzi.