Jumanne, 23 Septemba 2014

TIMU YA STENDI FC YAFUNDISHWA SOKA NA GHANA FC



Mashindano ya MALAFYALE CUP yameendelea katika  hatua ya 16 bora leo hii katika uwanja wa shule ya msingi mbata ikizikutanisha  timu mbili  GHANA FC na STENDI FC iliwachukua dakika kumi za kipindi cha kwanza kujipatia bao .dakika ya 42 kipindi cha kwanza  STENDI FC ilisawazisha na kuwafanya mashabiki wake kuendelea kushangilia dakika zote .kipindi cha pili kilianza kwa kila timu  kutawala lango la mwenzanke huku STENDI FC wakishambulia  lango la GHANA FC kama nyuki dakika ya 89 wachezaji wa GHANA FC na STENDI FC walipatiwa kadi nyekundu baada ya kutaka kupigana hadi filimbi ya mwisho inamalizika matokeo yalikuwa ni moja kwa moja ,ndipo maamuzi ya kupiga penati  tano  kwa kila timu ndipo GHANA FC wakiibuka na ushindi baada  ya STENDI FC kugongesha nguzo penati ya mwisho.