Jumanne, 30 Septemba 2014

AVEVA ATETA KUHUSU KUFANYA VIBAYA SIMBA




Rais Simba, Evans Aveva kwa mara ya kwanza amefungua mdomo wake na kulizungumzia suala la sare mbili katika mechi zao za Ligi Kuu Bara.
Aveva amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuungana na kuwa pamoja katika kipindi ambacho alikiita hawajapoteza wala kufanya vizuri.
Lakini akaenda mbali zaidi na kusema anamuamini Kocha Patrick Phiri, hivyo wampe muda kidogo kwa kuwa wanapita kwenye kipindi cha mpito. “Hatujafanya vibaya wala kufanya vizuri, sare mbili na hakuna mchezo tuliopoteza. “Ni suala la kujipanga ili kuangalia tutafanya nini katika mechi zinazofuatia. “Uongozi una changamoto nyingi, utaona tulifanya kila linalowezekana kwenye uchaguzi. “Baadaye kwenye usajili, lakini sasa bado mambo hayajakaa vizuri, ni suala la kupambana tu,” alisema Aveva