Jumatano, 24 Juni 2015

askari polisi kikosi barabarani watakiwa kurudi darasani kuongeza ujuzi

Kufuatia kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani jeshi la polisi kikosi cha usalama barabani nchini wamelazika kuwarudisha darasani askari wa kikosi cha usalama barabarani na kuwapa mafunzo ya ukaguzi wa malori na mabasi kwa vitendo katika chuo cha mafunzo ya ufundi veta ili kuwajengea uwezo wa kudhibiti  ajali barabarani.

Wakizungumza mkoani Morogoro askari wa ukaguzi wa malori na mabasi wamesema kufuatia kukua kwa sayansi na teknolojia ya vyombo vya usafirishaji serikali kupitia jeshi la polisi inatakiwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa maafisa na wakaguzi wa magari ili askari wake waweze kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ongezeko la ajali za barabarani.

Kaimu mkurugenzi wa mafunzo veta kanda ya mashariki Asanterabi Kanza akizungumza na wakaguzi hao wa malori na mabasi katika chuo cha elimu na mafunzo ya ufundistadi veta Kihonda mkoani Morogoro amesema idadi kubwa ya watanzani wamepoteza maisha kutokana na  ajali za barabarani ambazo baadhi yake zinasababishwa na wakaguzi kutokuwa na utaalamu wa kutosha kukagua magari ambapo amewataka wazingatie mafunzo ili kukabiliana na ajali zisizo la lazima.