Kitendawili
cha nani mbabe kati ya watani wa Jadi wa Msimbazi na Jangwani
kimekamilika baada ya Simba kufungwa bao 2-0 kwa mara ya pili ndani ya
miaka miwili, ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba
ambao walicheza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wake Abdi Banda
kupigwa kadi nyekunde hatua iliyodhoofisha zaidi nguvu ya wana Msimbazi.
Uzembe
wa mabeki wa Simba katika dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza ulipelekea
kupachikwa goli la kwanza na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe. Dakika ya
72 ya mchezo, uzembe wa mabeki wa Simba ulimpa nafasi mshambuliaji Amisi
Tambwe kucheka na nyavu zao.
Tambwe
ameiadhibu Simba, timu ambayo alimsajili kwa mara ya kwanza alipoingia
nchini na baadae kuhamia kwa wana Jangwani. Mchezaji huyo alipachika
goli huku walinzi wanne wa Simba wakiwa wanalandalanda katika eneo la
goli lao.
Yanga
wameweka historia ya kumfunga Simba kwa misimu miwili mfululizo huku
ikifuta machungu ya kushindwa kuifunga Simba kwa misimu 10 mfululizo
kati ya mwaka 2000 hadi 2009.