Alhamisi, 11 Februari 2016

Watu 11 Wafariki Dunia Muheza Tanga na Basi La Simba Mtoto

Ajali mbaya ya barabarani imetokea mkoani Tanga  leo asubuhi  wakati Basi la Kampuni ya Simba Mtoto ya Tanga lilipogongana na Lori uso kwa uso katika eneo la Pangamlima Wilayani Korogwe mkoani humo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukieo zinaeleza kuwa watu 10 wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya atika ajali hiyo.