WATU 12 wamepoteza maisha huku wengine 28 wakijeruhiwa leo baada ya
basi la New Force One kupata ajali eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo
mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanaume na wanne ni wanawake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanaume na wanne ni wanawake.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni
ya New Force One aina ya Youtong lenye namba za usajili T483 CTF
likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye
namba T 616 DEF katika kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoa wa
Iringa katika barabara kuu ya Iringa – Dar.
Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilula, kilomita 45 kutoka Iringa Mjini.
Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilula, kilomita 45 kutoka Iringa Mjini.