Jumapili, 8 Novemba 2015

STARS KUJIPIMA NGUVU JUMANNE NA TIMU YA AMAGLUG JUMANNE


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la Eldorado jijini Johannesburg.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaa katika uwanja wa Taifa na marudiano yake kufanyika Novemba 17 jiji Algiers kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Taifa Stars iliyokweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, baada ya kuwa na mazoezi ya stamina na pumzi kuweka uwiano sawa wa mazoezi (fitness level), Kocha wa Stars Charles Mkwasa sasa anaendelea na mazoezi ya kutengeza mfumo kwa wachezaji wake.
Awali Stars ilikuwa icheze mechi mazoezi leo Jumapili na timu ya University of Pretoria inayoshriki ligi kuu ya Afrika Kusni (PSL), lakini baada ya Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kuandaa mchezo  dhidi ya U23, sasa mchezo dhidi ya Tucks hautakuwepo.