Alhamisi, 11 Juni 2015

Serikali yatangaza Bajeti ya sh trilion 22.4 bila miradi mipya.

Serikali imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/16 ya shilingi trilioni 22, bilioni 495.5 na kuainisha maeneo ya ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi ikiwemo matumizi ya utaoji risit za kielekroniki katika mamlaka ya serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaa na wakala wa serikali.
Waziri wa fedha na uchumi Mhe.Saada Mkuya amesema hukusanyaji huo wa mapato yasiyo ya kodi utahusisha faini za mahakamani, faini za usalama barabarani, viingilio katika mbunga za wanyama, vibali vya kuvuna maliasili na kuwataka maafisa masuhuli kusimamia utekelezaji wa agizo hilo na kusisitiza mpango huo utasaidia kupunguza utegemezi wa fedha za wahisani.
 
Aidha amesema serikali imependekeza kuongeza tozo kwenye mafuta ya taa kutoka shilingi 50 kwa lita hadi shilingi mia moja hamsini kwa lita ili kuondoa uchakachuaji wa mafuta ambapo amesema kuwa hatua ya kuongeza tozo katika mafuta ya Petroli zinalenga kuongeza mapato ambayo yataelekezwa katika mradi wa usambazaji umeme vijijini. 
 
Akielezea shabaha ya msingi ya bajeti ya mwaka 2015/16 Mhe.Mkuya amesema kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya serikali za mitaa kufikia asilimia 13.1 ya pato la taifa ambapo matumzi ya serikali yanatarajiwa kuwa asilimia 20.6 ya pato la taifa na kuwa akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi matumizi ya bidhaa na huduma.
 
Aidha amesema katika bajeti ya mwaka 2015/16 inavipaumbele vichache ikiwemo kugharamia uchaguzi mkuu pamoja na gharama zote za bunge lijalo, kuweka msukumo katika miradi inayoendelea kwenye miradi ya umeme na maji vijijini na kuimarisha rasilimali watu.