Imeelezwa kuwa matanagzao ya Television kwa njia ya digitali yanaweza kuwa kichocheo cha kukuza uchumi endapo watoa huduma za Television watanzingatia maadili kwa kurusha vipindi vinavyolenga kuelimisha ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko hapa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na TCRA, Makamu wa Rais pamoja na masuala mengine amewataka watoaji huduma za Television kuhakikisha wanazingatia maadili ya kitanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kwa kuwa na vipindi vitakavyokuwa vikitoa elimu kama za afya.
Katika muhula wa nne wa utangazaji nchini zaidi ya Television 28 na Radio 104 zimekwisha kusajiliwa, ambapo waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema uwepo wa vyombo hivyo vya habari ni dhahili wizara, serikali pamoja na wananchi watarajie kuanza kupata mafanikio zaidi ya kiuchumi.
Licha ya Tanzania kuwa ya kwanza Afrika ya mashariki kuzima mitambo ya analojia, Zanzibar bado haijafanikiwa kuingia katika mfumo wa kidigitali kwani kwa mujibu wa mtendaji mkuu wa utangazaji Zanzibar anasema kumekuwa na changamoto nyingi huku kubwa ikiwa namna ya kufikisha mawasiliano hayo ya kidigiti vijijini.
Prof .John Nkoma ni mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania anasema masafa ya utangazaji kwa Television za Tanzania sasa yameongezeka.
Tanzania ilianza mchakato wa kuhama kutoka analojia kwenda digitali mnamo mwaka 2005 kwa kuwashilisha wadau ambapo hadi kufikia Dec 31 mwaka 2012, ilianza kuzima baadhi ya mitambo ya analogia kabla ya kuhama rasimi kutoka analojia hadi dijitali mnamo april 30 mwaka huu,
Katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali wandamizi wa serikali, TCRA iligawa tuzo za heshima ya digitali tanzania ambapo vituo vya ITV, EATV, na CAPITAL TV VILIPATA tuzo hizo.