Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na motto mwenye ulemavu wa ngozi, Kabula Zacharia, anayetunzwa kwenye kituo cha kulea watu wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija mkoani Shinyanga, mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini kufuatia kuchukua fomu za kuomba chama kimteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. . Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mh. Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wana CCM waliomdhamini mkoani Shinyanga, kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Shin yanga mjini Charles Sangula.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa.
Wana CCM waliofika kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015. Lowassa ambaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini,