Jumanne, 28 Aprili 2015
TEMI FELIX AMESEMA PRISONS WAJIPANGE TUMEJIPANGA KUWAFUNGA MAGOLI MENGI
Mshambuliaji mahiri wa City, Temi Felix amesema Prison wasitegemee mteremko kwenye mchezo ujao ligi kuu soka Tanzania bara kati ya timu hizo unaotarajiwa kuchezwa jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa mtandao wa club yake Temi atakayekuwa sehemu ya kikosi cha City baada ya kukosa michezo miwili iliyopita kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Yanga jijini Dar alitanabaisha kuwa Prison wajipange kupambana na wasitegemee mteremko katika mchezo huo kutokanana nafasi ya City hivi sasa kwenye msimamo wa ligi.
“Nadhani wanapashwa kujiandaa kuja kupambana uwanjani, bado tunakiu ya kushinda, tunataka kubaki kwenye nafasi ya nne ambayo pia ina zawadi, hakuna mteremko siko hiyo, tumejiandaa kuachapa bao nyingi tu” alisema Temi
Mshambuliji huyo wa City alikosa michezo miwili iliyopita kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya yanga jijini Dar, huku tayari akiwa ameifungia timu yake mabao 4 hadi hivi sasa.