Jumatano, 29 Aprili 2015

SKENDO NZITO KWA VIONGOZI MKOANI RUKWA


KATIBU Tawala Mkoa wa Rukwa na Watendaji wengine wanatuhumiwa kugawana magari ya Serikali zaidi ya Manne kwa matumizi yao binafsi.
Maofisa hao wa Serikali wamebainika kugawana magari hayo baada ya kuwasilisha taarifa ya Matumizi ya fedha za mkoa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali-PAC kwa ajili kupitiwa,ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo AMINA MWIDAU ameikataa na kudai ni chafu.
Mwenyekiti MWIDAU ameikataa taarifa hiyo mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo,ambapo wameonyesha kutoridhishwa na maelezo mbalimbali ya Maswali waliyokuwa wakiulizwa viongozi hao.