KIKOSI cha timu ya Mbeya City Fc kimefanya mazoezi ya mwisho jana tayari kwa kuivaa Azam Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara unaotarajiwa kuchezwa Chamanzi Complex ,Mbagala,Dar Es Salaam.
Akizungumza kuelekea mchezo huo Daktari mkuu wa City, Joshua Kaseko amesema kuwa mlinzi Yusuph Abdalah ‘Sisalo’ ataukosa mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata kwenye mcheo uliopita dhidi ya Ndanda Fc na nafasi yake itazibwa na Juma Nyosso ambaye tayari amemaliza kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi nane.
“Sisalo bado hali yake siyo nzuri, ni wazi hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo kwa sababu bado tunamtizamia, Juma Nyosso, amemaliza adhabu yake na kiafya yuko vizuri na imani Mwalimu Mwambusi atamjumuisha kikosini, kucheza dhidi ya Azam kunahitaji nguvu ya ziada binafsi sina wasiwasi tena na safu ya ulinzi baada ya urejeo wake” alisema.