Alhamisi, 2 Aprili 2015

Wajue Mastaa Watano Walionusurika Kufa Wakiwa Kazini



Kila kazi inautamu wake, lakini pia ina machungu yake. Pamoja na vipato vingi walivyojifunia kutokana na kazi zao zilizowapa umaarufu na heshima kubwa hapa dunia, hawa ni baadhi ya mastaa walionusurika kufa wakiwa kazini.
Jason Statham
Huyu ni muigizaji maarufu aliyetamba kwenye filamu nyingi nchni marekani. Jasoson alipata ajali alipokoswakuangukiwa na roli wakati akiigiza filamu ya Expendables 3.

Jackie Chan
Mcheza filamu wa kichina mwenye vituko ving Jackie Chan aliwahi kufanyiwa operesheni ya ubongo, baada ya kuumia vibaya kichwani wakati akiigiza filamu ya Armour of God.

George Clooney
Muigizaji huyu alitamani kujiuua yeye mwenewe hospitalini kutokana na kupata maumivu makali baada ya kuvunjika mgongo. George alipata ajali hiyo wakati akiigiza filamu ya Syriana.

Isla Fisher
Muigizaji huyu alijikuta akizama ndani ya maji na kushindwa kuibuka hewani kwa takribani dakika tatu. Tukio hilo lilitokea wakati akiigiza filamu ya Now You See Me.

Chevy Chase
Mchekeshaji maarufu Chevy Chase, alipata mshtuko wa umeme na kupoteza fahamu kwa muda. Ajali hiyo ilitokea wakati akiigiza filamu ya Modern Problems.