Moja kati ya mambo yanayowakosesha raha wachina kwenye michezo ni
timu yao ya soka kutofanya vizuri. Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu
kuhusu namna ya kuimarisha soka ya China na kuifanya timu ya taifa ya
wanaume ifanye vizuri, lakini matokeo bado si mazuri. Hali nzuri ni
kwamba hivi karibuni China imetangaza mpango wake wa kufanya mageuzi
katika mambo ya soka. Mageuzi hayo yana hatua 50, moja kati yao ni
kuufanya michezo wa soka kuwa somo rasmi shuleni. Hii itaweka msingi
mzuri katika kuondoa udhaifu wa soka ya China. Kwa sababu tunajua soka
huwa inaanza kwenye msingi, na huu si mchezo ambao mtu anaweza kujifunza
ukubwani.