Ijumaa ya February 20, Timbulo
ambae amezungumzia kisa alichokutana nacho mwaka jana alipoenda Mwanza
kwa ajili ya kufanya shoo, lakini wakati anafanya shoo maeneo ya Kahama
kuna promota mmoja aliyekuwa ameandaa shoo na baadhi ya wasanii lakini
hawakufika promota huyo akaamua kuzungumza na Timbulo
ili aende kwenye shoo hiyo ili kuziba pengo wakakubaliana akaanza
safari akiwa na dancer wake wawili, alipofika alikutana na promota huyo
na kuanza kufanya PA, baadae alimtaka amlipe hela zake kabla hajafanya
shoo lakini akawa anamkwepa na baadae akamkimbia, alipoona hivyo akamua
kuripoti Polisi kwa ajili ya usalama kutokana na watu ambao walikua
wameshalipa kiingilio kwa ajili ya shoo hiyo na kisha akaondoka.