Jumatano, 5 Agosti 2015

MAGUFULI ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR JANA,VIFIJO NA NDEREMO VYATAWALA

KWA HISANI MICHUZI BLOG
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia
Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada
ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam jana
ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM
na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.


Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza
Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi
 na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar
es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea
Urais


Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na
Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt
John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia
chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar 

 Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi
wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John
Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Urais kupitia chama
hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar