Jumamosi, 13 Juni 2015
BVR YAWA DILI KWA BAADHI YA WENYEVITI NA WATENDAJI MKOANI MBEYA
Wakazi wa kata ya maendeleo wameendelea kujitokeza katika vituo vya kujiandikishia vilivyopo maeneo ya Sokomatola jijini mbeya .Harubutz imewatembelea wakazi wa maeneo hayo na kutaka kujua huduma wanayoipata katika vituo vyao ni ya kulidhisha au hapana .wamesema siku ya jana ijumaa kuna matatizo madogo madogo ambayo ilikuwa kama ni kero kwao baada ya mashine za BVR kufanya kazi kwa kiwango cha chini na kufanya muda mwingi watu waendelee kukaa kusubili mpaka mashine ziweze kulekebishwa .mmoja ya vitu ambavyo Harubutz iliweza kuviona ni mpangilio mzuri wa kupanga foleni na kutokuwepo ugomvi kwa wakazi wa maeneo hayo pamoja na changamoto nyingi zilizopo .hata hivyo mmoja wa waatalamu wa mashine hizo za BVR ambaye akutaka jina lake liwekwe humu amesema kuna matatizo kwa viongozi wenyewe wa kata mbalimbali katika vituo vya kujiandikishia daftali la kudumu la wapiga kura kuchukua rushwa ndogo ndogo na kuwapa kipaumbele watu ambao wamewapa kitu kidogo na kujiandikisha pasipo kufuata utaratibu wa kupanga foleni katika maeneo mengi na kusababisha ugomvi baadhi ya maeneo ya kujiandikishia daftali la kudumu la kujiandikishia kupiga kura.