Kamati Kuu katika kikao
chake cha tarehe 22/05/2015 mjini Dodoma pamoja na mambo mengine
imepokea na kutafakari kwa kina taarifa ya maandalizi ya mchakato wa
kupiga kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa.
Baada
ya kutafakari na kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza
katika maandalizi hayo, Kamati Kuu ya CCM inaishauri serikali kwa
kushauriana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakizingatia changamoto
zilizopo na hali halisi ya mchakato huu, kutafuta njia muafaka ya
kulishughulikia na kulihitimisha jambo hili kwa maslahi mapana ya Taifa
letu.