Ijumaa, 17 Aprili 2015

etoile du sahel wawasili dar


Kuelekea mchezo wa Yanga na Etoile du sahel utakaopigwa katika uwanja wa taifa hapo kesho tayari timu ya Etoile du sahel imewasili jijini Dar es salaam katika hali isiyokuwa ya kawaida kocha wa timu hiyo amekataa kuongea na waandishi wa habari.
Nahodha wa timu ya Yanga Nadir Haroub Cannavaro kwa upande wake akizungumza  amesema mpira ni mchezo wa makosa hivyo wamejipanga vyema ili kuwezakufanya vizuri katika mchezo wa kesho
Naodha huyo pia akizungumzia timu kwa ujumla amesema wamejipanga vya kutosha kuhakikisha wanashambulia zaidi ili kuishinda mbinu ya wapinzani yao ya kuupozesha mpira pia amewataka watanzania kuoimbea dua Yanga kesha kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo wa kesho.