Jumamosi, 30 Mei 2015

Serikali yatakiwa kutoa maelezo kuhusu mabehewa 274 yaliyonunuliwa kutoka nchini india yakiwa machakavu.

Kambi ya upinzani Bungeni imeitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu  hatma  ya  mabehewa 274 ambayo yamenunuliwa na serikli  kutoka nchini india  yakiwa machakavu kwani yameligharimu taifa  Bilioni 200 na iache kuyatumia ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza  kutokea.
Akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani katika wizara ya uchukuzi  Mh.Moses Machali amesema mabehewa hayo yamelalamikiwa kwa kipindi  kirefu lakini serikali imeendelea kuwa bubu.
 
Wakichangia Bajeti hiyo baadhi ya wabunge wamesema siyo sahihi kila Mwaka serikali inatenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali lakini haipeleki fedha  hatua  ambayo inarudisha nyuma maendeleo.
 
Kamati ya kutatua migogoro na kupambamana na ajali ambayo ipo Bungeni limesema kukabiliana na ajali  kuna haja ya kuboreshwa zaidi kwa mipango iliyopo.
 
Awali akiwasilia Bajeti ya wizara yake Mh.Samweli Sitta amesema    wizara yake inamikakati mbalimbali ya kuboresha sekta ya usafiri   nchini ikiwemo kufufua sekta ya anga na reli ili kuhakisha maeneo yote  yanafikika.