Jumanne, 8 Machi 2016

Moto wawaka tena Iyunga sec



Mabweni mengine mawili ya shule ya Sekondari Iyunga iliyoko jijini Mbeya yameteketea kwa moto mchana huu.

Hii ni mara ya pili sasa moto kuzuka katika shule hiyo .Wiki kadhaa zilizopita moto ulizuka na kuteketeza bweni moja la Mkwawa(‪Pichani‬) huku sababu zikielezwa ni hitilafu ya umeme kutokana na uchakavu wa miundo mbinu shuleni hapo.

Jeshi la Zimamoto liko eneo la tukio kuukabili moto huo