Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo na kukuta mashine za CT Scan na MRI hazifanyi kazi.
Katika ziara hiyo aliyoifanya asubuhi ya leo, alikutana na mzee wa miaka 90 ambaye alikuwa akisubiri huduma hiyo tangu jana.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Wa Hospitali hiyo, Lawrence Museru, mashine hizo
ziliharibika tangu juzi na hivyo huduma zilisimama tangu jana asubuhi.
Tatizo
kubwa katika machine ya CT Scan picha hazisomeki vizuri na MRI
imeharibika spea ambazo kwa mujibu wa uongozi wa hospitali hiyo,
matengenezo yanaanza leo.
Hata
hivyo, Mwalimu ameagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa kuchukua
hatua madhubuti kuhakikisha kuwa mashine hizi zinarudi katika hali yake
ya kawaida.
Mashine
hizo zimeendelea kuwa changamoto kwa hospitali hiyo licha ya Rais John
Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta hali kama ya leo.