Jumapili, 2 Agosti 2015

UTARATIBU MBOVU WA KURA ZA MAONI ZA CCM JIMBO LA MBEYA MJINI YAZUA MENGI SIKU YA LEO KIGOGO HAUSISHWA KUMWAGA PESA KWA WAGOMBEA WAKE ILI ALINDE MASLAHI YAKE.

Matokeo ya Kura za maoni Mbeya mjini leo yamefanyika katika Kata 36 huku fitina za uchaguzi zikitawala kila pande.Viongozi wa Wilaya wahusishwa na mpango wa kuchakachua kura za maoni kwenye kata mbalimbali. moja ya viongozi ambao walibainika kusambaza ukabila ni Katibu wa Umoja wa wazazi wilaya ambaye yeye aliweza kusambaza ukabila wa kuwakataa wanyakyusa na wasafa na kusema sasa ni wakati wa kumpata mtu wa kabila tofauti na hayo makabila .lakini pia ni mpango madhubuti uliopangwa toka Mwaka 2012 na mmoja wa wagombea ambaye ni kabila tofauti na wanyakyusa na wasafa ,kutengeneza kambi ya vijana ambao aliongoza kwa kipindi chote iko kwa ajili ya kuweza kuwafundisha njia ya kuwamaliza wanasiasa  wenzake katika kipindi hiki moja ya Ajenda kubwa ambayo imebainika ni kutumia ujanja wa kuwambia wapiga kura mpigie namba hii na ukitoka unapatiwa kiasi cha shilingi elfu kumi ambacho vijana wengi jioni ya leo wamelalamikia kitendo hicho cha kuzulumiwa haki yao huku tayari wakiwa wamepiga kura,pia Mtandao huu ulibahatika kuongea na baadhi ya wagombea ambao wao wamelalamikia vitendo vichafu vilivyofanywa na mgombea mwenzao ambaye wamesema wao hawana la kusema wanasubili majibu toka kwenye vikao vya chama .lakini pia kuna wasiwasi wa chama kupasuka endapo matokeo yatakwenda ndivyo sivyo.hadi hivi sasa hakuna kulala ila kazi ipo kwa wagombea watatu Aman kajuna ,Sambwee shitaambala,na charles mwakipesile lazima kieleweke mmoja wao ambaye atashinda .hata hivyo Mtandao huu umebaini moja ya kigogo aliyeachia ngazi kugombea Ubunge kwenye jimbo lake baada ya kudondoka nafasi ya urais ndiye aliyewapa vijana wake goli la mkono  wagombee nafasi za Ubunge ili walinde maslahi yake, pia Mtandao huu umebaini mchezo wa haraka haraka ulifanyika kuwatoa baadhi ya makatibu kuwapeleka mikoa mingine na kuwaleta makatibu wao wengine ili waweze kwenda sambamba na Wagombea wao.