AZAM FC Leo imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, walipoitoa Yanga kwa Penati 5-3 kufuatia Sare ya Dakika 90 ya 0-0 katika Mechi ya Robo Fainali iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano, Kipa wa Azam FC Aishi Manula aliokoa Penati iliyopigwa na Mwinyi Mngwali na Aggrey Morris kuifungia Azam FC Penati ya mwisho na kuipa ushindi.
Penati nyingine zilipigwa na kufungwa na Kipre Tchetche, Wawa, John Bocco na Himid Mao kwa Azam FC wakati za Yanga zilifungwa na Nadi Haroub 'Cannavaro', Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.
Mapema, katika Mechi nyingine ya Nusu Fainali, KCCA ya Uganda iliitoa Al Shandy ya Sudan Bao 3-0 na pia kutinga Nusu Fainali.
Kwenye Nusu Fainali hapo Ijumaa, Gor Mahia ya Kenya itapambana na Al Khartoum ya Sudan wakati Azam FC itacheza na KCCA.
Nusu Fainali hizi zitakuwa kama marudio ya Mechi za Makundi kwani Timu hizo zilipambana kwenye Makundi yao kwa Azam FC kuifunga KCCA 1-0 kwenye Kundi C na toka Kundi A Gor Mahia kutoka 1-1 na Al Khartoum.