Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendeshwa na kampuni ya
Proin Promotion linalolenga kuinua vipaji kwa vijana ikiwa ni katika
kuwatengenezea mazingira ya ajira katika maisha yao Nchi nzima kikanda
lionekana kuwa msaada kwa vijana wengi waliokuwa wakijitokeza kushiriki
mashindano hayo katika mikoa mbalimbali tulikopita.Shindano
la ya Tanzania Movie Talents msimu wa pili 2015 lilioanza mwezi Aprili
kikanda kwa kuanza na kanda ya ziwa mwanza, Kanda ya kaskazini
Arusha,Kanda ya kati Dodoma na kisha kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya
limekamilika kwa siku ya jana kupatikana washindi watatu na
kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano kila mmoja kati ya washiriki
mia tatu waliojitokeza kushindanaJana
jioni Jijini Mbeya Soko Matola Mkapa Conference Center ndipo mashindano
hayo yalipofanyika na kuhudhuliwa na vijana kutoka wiraya zote za mkoa
wa Mbeya na mikoa ya jirani kama Iringa na mikoa mingine ya jirani.
Washindi
hao watatu watakwenda kuungana na wenzao wa kutoka kanda zote nchini
kwa kuingia kwenye nyumba ya TMT wakifundishwa sanaa na waalimu mbali
mbali kutoka Chuo kikuu Mlimani,kisha kuwepo na mtoano wa kila wiki
ilikubaki washiriki kumi na mwisho kupata mmoja atakayeibuka na shilling
Milioni Hamsini za kitanzani,hao kumi watakao baki wataigiza movie ya
pamoja ikiwa ni katika kuwatambulisha katika tasni ya sanaa nchini ili
iwe ajira kwako.Baada ya kutoka Jijini
Mbeya ni Mtwara tarehe 26 na 27 mwezi huu kisha Dar es salaam 5-7 mwezi
wa 6,kwa taraifa zaidi tazama ITV na sikiliza Redio one au redio za mkoa
husika kujua taharifa zaidi za mahala na muda.